Elimu ndio njia ya pekee itakayopelekea kumalizwa kwa visa vya ukeketaji miongoni jamii zinazoendeleza tamaduni hiyo ambayo imepitwa na wakati
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kupambana na ukeketaji katika eneo la Alale Pokot Kaskazini gavana John Lonyangapuo anasema changamoto kuu ya kubali tamaduni hiyo ni ukosefu wa elimu miongoni mwa wanajamii ambao wamekuwa wakidhamini mila na itikadi bila kufahamu umuhimu wa elimu katika maisha ya baadaye
Lonyangapuo amekariri kujitolea kwa serikali yake kufanikisha juhudi za kuondoa ujinga na umaskini kupitia manifesto yake ambayo ni elimu usawa na kuimraisha uchumi ili kuafikia malengo ya kubadilisha taswira ya watu kuhusu kaunti ya Pokot Magharibi.
Kwa upande wake mkewe Mary Lonyangapuo ameelezea haja ya juhudi za pamoja miongoni mwa wanajamii ili kumaliza ukeketaji na kutimiza malengo ya serikali kumaliza utamaduni huwo kufikia mwaka wa 2022.