Maafisa wa Polisi katika Kaunti ya Trans Nzoia wanakichunguza kisa ambapo mwanamume wa umri wa miaka 35 amekatwa kwa panga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Ijumaa kwenye kijiji cha Matecha katika mtaa wa mabanda ya Tuwan viungani mwa mji wa Kitale.
Shangazi wake, Jeniffer Wamugune ameiambia North Rift Radio kwamba aliuliwa kikatili nje ya mlango wake wakiwa wamelala.
Wanakijiji nao wamekishtumu kisa hicho na kuvirai vyombo vya usalama kuzidisha doria nyakati za usiku sawa na kufanya uchunguzi wa kina kuwatia nguvuni watakaopatikana kuutekeleza uovu huo.