Polisi kaunti ndogo ya Marigat kaunti ya Baringo wametekeza zaidi ya mashine 50 za kamari baada ya akina mama kuibua madai kwamba waume zao na vijana wa ndogo wameathirika na mchezo wa kamari.
Akina mama hao waliokuwa na ghadhabu wamesema familia nyingi zimevunjika baada ya wanaume wengi eneo la Marigat kushindwa kutoa mahitaji ya msingi kwa familia zao kwani wengi wao wamekuwa wakiiba vyombo vya nyumbani na kuuza ili wapate pesa za kutumia kishiriki michezo ya kamari.
Akizungumza wakati wa kuteketeza vifaa hivyo Afisa mkuu wa polisi eneo la Marigat Maalim Mohammed amesema wamepokea lalama nyingi kutoka kwa wananchi kuhusiana na uwepo wa mashine za kamari licha ya serikali kupiga marufuku michezo hiyo huku akiwataka wanaume eneo la Marigat kutafuta mbinu nyingine ya kuingiza kipato badala ya kutegemea michezo ya kamari kama kitega uchumi
Hata hivyo Maalim amesema kwamba Afisi yake itahakikisha wakaazi wa Marigat wanafanya kazi inayowaingizia kipato kwa njia halali badala ya kutegemea michezo ya kamari kuchuma riziki.
Ikumbukwe michezo ya kamari kaunti ndogo ya Marigat imechangia visa vya uhalifu kuongezeka lakini pia imepelekea wanafunzi wengi kuacha masomo hasa katika mtaa wa kambi Turkana na viunga vyake.