Nyota wa muziki nchini Otile Brown amewataka wasanii nchini kutokubali kupewa shinikizo na watu kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwalinganishwa na wasanii waliowazidi kimuziki kutoka mataifa mengine.
Kupitia post ndefu aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kisha akaifuta Otile Brown amesema amechoshwa na kasumba ya watu kwenye mitandao kuwashindisha wasanii wa Kenya na wasanii wengine wenye mafanikio makubwa kimuziki ikizingatiwa kuwa wasanii wengi nchini hawana watu wa kuwafadhili na kusimamia kazi zao.
Mkali huyo wa ngoma ya Dusuma amewataka wakenya kutowapa wasanii shinikizo zisozo kuwa na msingi kwani wengi wao wanajituma kwenye suala la kutoa muziki mzuri na kuupeleka muziki wa Kenya kimataifa.