NI AFUENI KWA WAZAZI TURKANA NDOGO YA KATI BAADA WAKFU WA LODEPEE FOUNDATION KUTOA MSAADA KWA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

NI AFUENI KWA WAZAZI TURKANA NDOGO YA KATI BAADA WAKFU WA LODEPEE FOUNDATION KUTOA MSAADA KWA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

Wazazi katika kaunti ya ndogo ya Turkana ya kati sasa wamepata afueni baada ya mbunge wa eneo hilo kupitia wakfu wake wa Lodepee Foundation kutoa vifaa vya masomo vya takriban shillingi millioni tatu kwa wanafunzi ambao wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Akizungumza kwenye hafla ya kugawa vifaa hivyo mjini Lodwar, mbunge wa turkana ya kati John Lodepee amesema mpango huo wa kuinua masomo kwa wenyeji utafaidi wanafunzi zaidi ya 300 ambao kwa sasa wanajianda kujiunga  na kidato cha kwanza.

Aidha Lodepee ametoa wito kwa wahisani kupiga jeki juhudi za wakfu wa Lodepe Foundation kufadhili wanafunzi kimasomo ili kuinua viwango vya elimu katika kaunti ya Turkana.

Ni kauli ambayo imekaririwa na Waziri wa Elimu kaunti ya Turkana Patrick Losike akisema serikali kaunti ya Turkana inatambua juhudi za wadau wa elimu ambao wamehamua kuinua viwango vya masomo kaunti hiyo kupitia misaada ambayo wanatoa kwa familia ambazo hajiwezi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Ekwee Ethuro ameitaka Tume ya Kuajiri Walimu  Nchini TSC kuwaajiri walimu zaidi kaunti ya turkana kwani kaunti hiyo inashuhudia uhaba mkubwa wa walimu wa shule za msingi na upili.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts