Serikali ya kaunti ya Turkana imetia sahihi mkataba wa maelewano na ubalozi wa uholanzi nchini kuhimarisha ushiriki wa sekta ya kibinafsi katika kuwekeza kwenye ukuaji wa sekta ya umma ili kuafikia malengo endelevu.
Akizungumza mjini Lodwar kwenye mkao na balozi wa uholanzi nchini gavana wa kaunti ya turkana Josphat Nanok amesema mkao huo umepelekea kuzinduliwa kwa mpango wa prospects ambao unalenga kupiga jeki misaada ya kibinadamu na maendeleo kaunti hiyo hasa kwenye sekta ya elimu na nyanja zingine za kimaendeleo.
Nanok amesema serikali ya kaunti ya turkana ipo tayari kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo kufanikisha utekelezwaji mpango huo unaonuia kuwafaidi wakaazi wa kaunti hiyo.
Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi Maarten Brouwer ameeleza kuwa serikali ya uholanzi iko tayari kushirikiana na kaunti ya turkana katika kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi na kuhakikisha utekelezwaji wa mpango wa maendeleo na kiuchumi wa kalobeyei unawafaidi wakimbizi na wakaazi kaunti hiyo kupitia mpango wa prospects.