MWIMBAJI THE WEEKND AZITEMA RASMI TUZO ZA GRAMMY

You are currently viewing MWIMBAJI THE WEEKND AZITEMA RASMI TUZO ZA GRAMMY
  • Post category:Burudani

Msanii wa muziki wa Pop duniani the weeknd ameweka wazi uamuzi wake wa kutopeleka nyimbo zake kwenye tuzo za Grammys baada ya kutoteuliwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu.

Katika mahojiano yake na jarida la newyork times the weeknd amesema kwamba hatowasilisha nyimbo zake tena kwa ajili ya kufikiriwa kwenye tuzo hizo na ameionya label yake pia kutofanya hivyo.

Ni miezi mitatu imepita baada ya the weeknd na Grammys kupishana kauli baada ya waandaaji wa tuzo hizo kuto kuhusisha nyimbo zake wala album katika vipengele vya tuzo hizo kwa mwaka huu licha ya album yake ya ‘After Hours’ kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali sambamba na wimbo wake “Blind Lights” kufanya vizuri pia.

Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Grammys mwaka wa 2021 itafanyika huko Los Angeles Jumapili hii machi 14

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa