HATUA YA MAHAKAMA KURUHUSU KATIBU WA KNUT WILSON SOSSION YASHABIKIWA NA WADAU WA ELIMU,TURKANA.

HATUA YA MAHAKAMA KURUHUSU KATIBU WA KNUT WILSON SOSSION YASHABIKIWA NA WADAU WA ELIMU,TURKANA.

Siku moja baada ya Mahakama ya Leba kuamuru Wilson Sossion kuendelea kushikilia wadhifa wa ukatibu mkuu wa Chama cha Walimu Nchini KNUT,Mwenyekiti wa chama cha KNUT tawi la Turkana Bwana Kenyaman Eriong’oa ameshabikia hatua hiyo akisema kwamba ni ushindi mkubwa kwa walimu wa kenya.

Akizungumza na wanahabari mjini Lodwar, Eriong’oa amesema uamuzi wa mahakama ni afueni kwa chama cha KNUT ambacho katika siku za hivi karibuni kimekumbwa na misusuko baada ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutaka kumtimua Wilson Sossion kwenye wadhfa wake wa ukatibu mkuu.

Aidha Eriongoa amewataka viongozi wa kitaifa wa chama cha knut ambao wamekuwa wakishinikiza kubanduliwa kwa sossion kutafuta suluhu la kudumu kwa njia ya mazungumzo kutatua mgogoro ambao umekuwa ukizingira chama hicho.

Wakati huo huo amekinyoshea kidole cha lawama Tume ya Kuajiri Walimu Nchini TSC kwa kile anachokidai kuwa tume hiyo imekuwa ikijaribu kulemaza juhudi za Chama cha Walimu nchini KNUT ya kupigania haki za walimu.

Hata hivyo  Eriong’oa amewataka walimu kwenye kaunti ya Turkana kuendelea na shughuli za kimasomo bila wasiwasi wote kwani kwa sasa Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Bwana Wilson Sossion amepata afueni baada ya mahakama kutupilia mbali kesi ya kumtaka abanduliwe kwenye wadhfa wake.

 

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts