MWANAMUZIKI MKONGWE WA RHUMBA,JOSKY KIAMBUKUTA AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 72.

You are currently viewing MWANAMUZIKI MKONGWE WA RHUMBA,JOSKY KIAMBUKUTA AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 72.
  • Post category:Burudani

Msanii nguli wa muziki wa Rhumba kutoka DR. Congo Josky Kiambukuta Londa amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72 huko Kinshasa.

Kwa mujibu wa Familia yake, Kiambukuta alifariki mapema leo baada ya kuugua kwa muda katika Hospitali ya Ngaliema iliyoko Jijini Kinshasa.

Josky Kiambukuta Londa alizaliwa Februari 14 mwaka wa 1949 huko Kinshasa nchini DRC Congo ambako alianza muziki mapema miaka ya 1960 alipojiunga na Bendi ya TPOK Jazz chini ya uongozi wa Franco Luanzo Luambo Makiadi.

Akiwa chini ya kundi la TPOK Jazz kati ya miaka ya 1960 na 1980, Josky Kiambukuta alipata umaarufu mkubwa kwenye muziki wa Rumba alipoachia nyimbo kali kama Missile, Chandra, Ayez Pitie,Selengina, Aziza, Likambo Moto te, Reciprocite Sula na nyingine kibao.

Baada ya kifo cha Franco mwaka wa 1989, Josky Kiambukuta aliendelea kuwa member wa kundi la TPOK Jazz kwa miaka minne hadi mwaka wa 1994 wakati bendi hiyo ilipovunjika baada ya mgogoro kuibuka kati yao na familia ya Franco kuhusiana na mapato ya nyimbo za bendi ya TPOK Jazz.

Kutokana na hilo, Josky Kiambukuta pamoja na member wenzake wakiongozwa na Simaro Masiya Lutumba na Ndombe Opetum, waliunda bendi yao iitwayo Bana OK na wakaachia album kadhaa zilizokonga nyoyo za wapenzi muziki wa Rhumba duniani ikiwemo Kilo ya Kinshasa ya mwaka wa 1998 na Bula Ntulu ya mwaka wa 2002.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa