Kundi la watu wenye ulemavu katika Kaunti ya Trans Nzoia limeelezea wasiwasi wake kwa kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata ulemavu wengi wao wakiwa wanabodaboda.
Mwenyekiti wa Vijana wa Watu Wenye Ulemavu, Ojiambo Opis amesema wengine wa waendeshaji pikipiki wanaohusika kwenye ajali wameishia kukatwa miguu na baadhi yao kuwekewa vyuma kurejelea hali yao ya kawaida.
Kufuatia hilo Opis amesema wameanzisha kampeini ya kuhamasisha wanabodaboda kuhusu umuhimu ya kuzingatia sheria za trafiki, kuacha kutumia vileo wakiwa kazini na kuwaondoa watoto katika sekta hiyo.