Tee billz ambaye ni mume wa zamani wa Tiwa Savage anaamini hakuna msanii yeyote wa kuanzia mwaka wa 1900 hadi 2021 ambaye anaweza kumshinda mke wake wa zamani kwenye muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tee billz amesema kama kuna mtu anajiamini anaweza kushindana naye ajitokeze na akimshinda msanii huyo atampa dola milioni 1.
Tee billz na Tiwa savage walioana November 23 mwaka wa 2013, na mwaka 2015 wakabarikiwa kupata mtoto wa kiume aitwaye “Jamil Balogun” lakini mwaka wa 2016 wawili hao walitangaza kuachana.