Mtu mmoja ameaga dunia huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali ya barabarani, Kaunti ya Turkana.
Akithibitisha tukio hilo Afisa wa polisi Kaunti Ndogo ya Turkana ya kati Canningham Suiyenga amesema ajali hiyo imetokea baada ya gari lilokuwa likitoka Lodwar likielekea Kakuma kupoteza mweelekeo na kubiringika mara kadhaa, gurudumu lake lilipopasuka likiwa safarini.
Suiyenga amewasihi madereva kuwa waangalifu na kuzingatia sheria za barabarani ili kupunguza uwezekano wa ajali kutokea.
Hata hivyo aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo kwa sasa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya misheni ya Kakuma huku mwili wa aliyeaga dunia ukihifadhiwa katika ya hospitali ya Rufaa ya Lodwar.