Sasa ni rasmi kwamba watahiniwa wa darasa la 8 na kidato cha nne wataanza mtihani wao wa kitaifa katika kipindi cha wiki 8 zijazo.
Waziri wa Elimu Prof. George Magoha amesema kuwa wanafunzi wa darasa la nane wataanza mtihani wao tarehe 19 mwezi Machi huku wale wa kidato cha nne wakianza tarehe 25 mwezi Machi akisema akiwataka watahiniwa kujiepusha na visa vya utovu wa nidhamu na kuweka juhudi zao kwa masomo.
Aidha Magoha amesema huenda serikali ikalazimika kurejesha adhabu ya viboko kufuatia kukithiri kwa visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.
Hata hivyo amedai visa vinavyoshuhudiwa kwa sasa nchini hasa uteketezaji wa shule na uharibifu wa mali vinaweza kuwa vimechangiwa na hatua ya kutowaadhibu wanafunzi.