Msanii wa muziki wa Dancehall kutoka Weasel Manizo amewashauri wasanii wapya, Eezy wa ngoma ya Tumbiza Sound na Mudra, hitmaker wa Muyayayu kutopumzika iwapo wanataka kubaki kwenye kiwanda cha muziki nchini humo kwa muda mrefu.
Kwenye moja ya interview, Weasel amesema wasanii wanaochipukia wanapaswa kusikiliza aina tofauti za muziki ili kupata msukumo wa kutoa muziki mzuri.
Aidha mkali huyo amewashauri kushirikiana na wakongwe wa muziki nchini uganda kwa kuwaheshimu kila wakati badala ya kufikiria kwamba wao ndiyo bora zaidi.
Ikumbukwe Weasel alikuwa na ukaribu sana na msanii redio ambaye walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja kwenye good life crew lakini tangu kufariki kwa msaani huyo mashabiki kadhaa wa muziki na wakosoaji nchini Uganda hakuwa na Imani nae lakini mwisho wa siku alifanikiwa kujisamamia kama msanii wa kujitegemea.