Msanii wa Sol Generation, Bensoul amejiunga rasmi na baadhi ya watu nchini wanaoshinikiza kuhalalisha kwa bangi.
Akipiga stori kwenye kipindi cha Bonga na Jalas, Mkali huyo wa ngoma ya Nairobi amesema kwamba kuhalalisha kwa mmea huo kutasaidia kukuza uchumi wa Kenya.
Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kuwa bangi humsaidia kufanya kazi zake kwa umakini bila ya kuchoka.
Bensoul anajiunga na msanii mwenzake Octopizzo pamoja na seneta wa Narok Ledama Olekina ambao wamekuwa wakishinikiza kuhalalishwa kwa bangi nchini