Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini Nigeria Omah Lay amedokeza kuwa yuko tayari kutumbuiza tena nchini Uganda ikiwa atapata nafasi.
Kwenye mahojiano na Redio moja huko Lagos, nchini Nigeria, hitmaker huyo wa “Bad Influence” amesema anaifanyia kazi albamu yake mpya ambayo inazungumzia tukio la kukamatwa kwake nchini Uganda.
Aidha amethibitisha ikiwa mapromota wa muziki nchini Uganda watazungumza na uongozi wake,hana budi kurudi kutumbuiza nchini humo.
“Sijuti kukamatwa huko Uganda, nilijifunza mengi kutokana na tukio nzima. Natumai nitatumbuiza tena pande hizo, naifanyia kazi albamu yangu mpya ambayo inazungumzia matukio yote yaliyonikuta nchini Uganda,” amesema kwenye mahojiano.