MSANII SLEJJ AKANUSHA STORI ZA MKE WA DADDY OWEN KUOLEWA NA BWENYENYE MMOJA HUKO GILGIL.

You are currently viewing MSANII SLEJJ AKANUSHA STORI ZA MKE WA DADDY OWEN KUOLEWA NA BWENYENYE MMOJA HUKO GILGIL.
  • Post category:Burudani

Msanii wa nyimbo za Injili nchini Owen Mwatia maarufu Slejj amenyosha maelezo kuhusu ishu ya kuvunjika kwa ndoa ya kakake Daddy Owen kwa kusema kuwa mke wa Owen hajaolewa na mwanaume mwingine kama ambavyo vyombo vya habari nchini vinaripoti.

Slejj ameshutumu vyombo vya habari nchini kwa kueneza habari za uongo akisema kwamba, Daddy Owen na mkewe Farida walikuwa na ugomvi wa kinyumbani kama mke na mume lakini hawajatengana.

Aidha amedai kuwa kama familia, wamezungumza juu ya kile kilichotokea kati Daddy Owen na mkewe ambapo kwa sasa kila kitu kipo shwari kwani wawili hao wamemaliza tofauti zao.

Ikumbukwe Siku chache baada ya vyombo vya habari nchini kuripoti kuwa Farida ameolewa na bwenyenye mmoja huko Gilgil, Daddy Owen alitoa taarifa akisema kwamba amekuwa akipitia wakati mgumu kwa siku chache zilizopita kufuatia ukweli wa habari kuwaa ndoa yake ilikuwa njia panda.

Hitmaker huyo wa Vanity alitumia fursa hiyo kuwasihi mashabiki wake wamuombee kwani alikuwa anapitia msimu wenye changamoto nyingi lakini hakuthibitisha au kukataa kama kweli mkewe alikuwa ametoka nyumbani kwake au kama alikuwa ameposwa na mwanaume mwingine.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa