Facebook, Twitter, YouTube na Snapchat zinapambana kuondoa filter ya Silhouette Challenge baada ya kuanza kutumika vibaya mitandaoni.
Ni challenge ambayo ilianza hivi karibuni ambapo watumiaji wanatumia rangi nyekundu na nyeusi kuficha muonekano na kurekodi video fupi ambazo nyingi hazipo katika maudhui mazuri.
Challenge hii haikuanza kwa lengo la kuhamasisha vitendo vya kijinga, bali ilianzishwa na Clementine Ford ikitumia wimbo wa zamani wa Doja Cats kama style yake ya kuficha taarifa za video ili kuweza kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake. Sasa hivi inatumika vibaya na watu wengi ikionyesha vitendo na dancing ambazo sio nzuri kimaudhui.
Hata hivyo YouTube, Twitter, Facebook na Snapchat zinapambana kufuta video chafu zilizovuja zikionyesha watu waliotumia kujificha kwa kutumia filter hii, zikibadilishwa na kuonyesha taarifa bila rangi nyekundu na nyeusi. Hivyo inafichua sura na maumbo ya mtu anayecheza.
MITANDAO MIKUBWA YA KIJAMII DUNIANI KUONDOA FILTER YA SILHOUETTE CHALLENGE
