MISAADA ZAIDI ZATOLEWA KWA WAATHIRIWA WA MKASA WA MAPOROMOKO YA ARDHI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Waathiriwa wa mkasa wa maporomoko ya ardhi eneo la Nyarkulian, Muino na Parua kaunti ya Pokot Magharibi wamepokea shilingi milioni 6.2 kutoka kwa benki ya Kenya Commercial Bank KCB,

Akizungumza alipompokeza gavana wa jimbo la Pokot Magharibi John Lonyangapuo na hundi ya shilingi milioni 6.2 mkurugenzi wa benki ya KCB Anastasia Kimtai anasema kwamba fedha hizo zitafadhili mabati kwa familia zote athirika.

Kando na kutoa msaada kwa waathiriwa kimtai anasema zaidi ya makundi 12 kaunti ya Pokot Magharibi imefaidika na mpango wa huduma za biashara na maendeleo.

Kimtai vile vile amesema benki ya KCB itawapa wasichana 100 kutoka kaunti ya Pokot Magharibi mafunzo kuhusu kilimo biashara chini ya mpango wa global give back circle.

Alex Toilem

Alex Toilem is a kiswahili news anchor, news editor at Northrift Radio 104.9 and 104.5 fm He is also

Related Posts