MESSI AFUNGIWA MECHI TATU BARCELONA

You are currently viewing MESSI AFUNGIWA MECHI TATU BARCELONA
  • Post category:Michezo

Nahodha wa klabu ya Barcelona muargentina Lionel Messi amejikuta katika adhabu ya kutocheza michezo miwili ya ligi ya Hispania na mechi moja kombe la Copa Del Rey akiwa na klabu yake ya Barcelona.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya Messi kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 120 katika finali ya Supercopa De Espana dhidi ya klabu ya Athletic Bilbao.

Messi alioneka katika kamera za marejeo (VAR)akimchezea mchezo ambao sio wakiuungwa mchezaji wa Athletic Bilbao Asier Villalibre huku Barcelona wakimaliza mchezo kwa kula kichapo cha goli tatu kwa mbili.

Hivyo Messi ataukosa mchezo dhidi ya Cornella katika mshindano ya Copa del Rey,Elche na baadae mechi ya mwisho dhidi ya Athletic bilbao kwamara nyingine tarehe 31 Januari.

Sasa kwa Lionel Messi hii inakuwa kadi yake nyekundu ya 3 katika maisha yake ya soka kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa katika miaka yake yote 17 soka na inakuwa kadi nyekundu ya kwanza kwa ngazi ya klabu yaani Barcelona.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa