MCHAKATO WA KUKUSANYA MAONI KUHUSU MSWADA WA BBI KUTOKA KWA WANANCHI UMEANZA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

You are currently viewing MCHAKATO WA KUKUSANYA MAONI KUHUSU MSWADA WA BBI KUTOKA KWA WANANCHI UMEANZA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Wakaazi wa Kaunti ya Pokot Magharibi wametakiwa kujitokeza katika maeneo tofauti kutoa maoni yao kuelekea mchakato wa kupasisha ripoti ya maridhiano BBI.

Spika wa Bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi anasema zoezi la kupokea maoni ya Wananchi itaendelea katika maeneo Bunge yote manne huku Wawakilishi wa Wadi wakizuru maeneo hayo kuzungumza na Wananchi.

Mukenyang anasema Bunge hilo litazingatia zaidi maoni yanayotolewa na Wananchi kabla ya kuafikia uwamuzi wa kuupasisha au kuangusha Mswada huwo.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.