MASHABIKI WA KLABU YA MANCHESTER UNITED TAWI LA LODWAR WAMETUMIA SIKU YA WAPENDANAO DUNIA KUWASAIDIA WANGOJWA

MASHABIKI WA KLABU YA MANCHESTER UNITED TAWI LA LODWAR WAMETUMIA SIKU YA WAPENDANAO DUNIA KUWASAIDIA WANGOJWA

Huku ulimwengu ikiadhimisha siku ya Valentines day hii leo, mamia ya mashabiki wa timu ya Manchester United tawi la Lodwar wamesherekea siku hii kwa njia ya kipekee kwani wamehamua kutumia siku ya wapendanao kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Lodwar na kuwapa msaada.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Tim Timmoh ambaye ni mmoja wa viongozi wa mashabiki wa klabu ya Manchester katika kaunti ya Turkana amesema kampeini hiyo walilolipa jina la Red with A Purpose lililenga kuwatembelea wagonjwa na kutoa zawadi ya damu kwa watu wenye uhitaji wa bidhaa hiyo adimu.

Akizungumza kwa niaba ya hospitali ya rufaa ya Lodwar mshirikishi wa kitengo cha damu katika hospitali hiyo Samuel Kapengi ameshabiki hatua ya wafuasi ya timu ya Manchester United tawi la Lodwar kushirikiana nao kwenye shughuli ya kuchanga damu ikizingatiwa kuwa kuna idadi kubwa ya watu wenye uhitaji wa damu katika kaunti yaTurkana.

Hata hivyo ametoa wito kwa wahisani wengine kujitolea na kushirikiana nao kwenye shughuli ya utoaji damu ili kukithi idadi kubwa ya watu wanaohitaji damu katika hospitali ya rufaa ya Lodwar kwani imebainika akina mama na watoto ndio wanahitaji bidhaa hiyo adimu kwa wingi.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts