Usalama umeimarishwa katika jengo la Bunge la Marekani kufuatia taarifa za kuwepo na njama za uvamizi.
Kutokana na hali hiyo, Baraza la Wawakilishi limesitisha ratiba za leo, lakini Seneti itaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, imeelezwa kuwa Kundi la Wanamgambo lilipanga kufanya hayo leo Machi 04, siku ambayo Marais walikuwa wanaapishwa.
Tishio hilo linakuja miezi miwili baada ya ghasia za wafuasi wa Donald Trump kutokea kufuatia Rais huyo wa zamani kushindwa Uchaguzi Mkuu