MAMIA WANUFAIKA NA KAMBI YA MATIBABU YA MACHO,KAUNTI NDOGO YA LOIMA

MAMIA WANUFAIKA NA KAMBI YA MATIBABU YA MACHO,KAUNTI NDOGO YA LOIMA

Zaidi ya wakaazi 100 kwenye hospitali ya Lorughum Kaunti ndogo ya Loima wamepata matibabu ya macho bure ambapo wengine zaidi ya 53 wamefanyiwa upasuaji wa macho baada ya kubainika kuwa wana tatizo la kutoona vizuri

Akizungumza na meza yetu ya habari, Msimamizi wa timu ya wataalam wa Afya waliotumwa kwenye hospitali ya Lorughum kutoa huduma za matibabu ya macho Dakta Ekiru Kidalio,amesema hatua hiyo ililenga kuwasaidia walio na shida za kiafya na wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu.

Wakati huo huo baadhi ya wananchi waliopatiwa matibabu ya macho wamefurahishwa na hatua hiyo wakitoa shukhrani kwa wasimamizi wa matibabu hayo kwa kile walichodai kuwa wamepata huduma bora.

Hata hivyo kidalio amewataka wakaazi wa Kaunti ndogo ya Loima kujitokeza kwa wingi kwenye kambi nyingine ya matibabu ambayo itafanyika tena kwenye hospitali ya lorughum ili waweze kufaidi na matibabu ya bure kwa mangonjwa mbali mbali yanayowasibu.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts