Mtayarishaji wa muziki nchini, Magix Enga amenukuliwa akimuita msanii wa muziki nchini, Arrow Boy ‘mshamba’ baada ya msanii huyo kutaja gharama za video ya wimbo wake mpya, uitwao ‘Fashionista’.
Arrow Boy alisikika katika mahojiano na kituo cha redio cha humu nchini akidai kuwa video ya wimbo wake huo imegharimu shillingi millioni 2.2.
Mbali na kumuita Arrow Boy, mshamba katika video hiyo, Magix Enga pia aliweka mtandaoni screenshot ya mazungumzo aliyofanya miezi kadhaa na msanii huyo bila majibu akimtaja kuwa alishindwa kulipia gharama za huduma za studio alizompa.
Hata hivyo Arrow Boy amekana madai yaliyoibuliwa na Magix Enga akisema kuwa hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa alishalipa gharama zote za kutayarisha wimbo wake wa “Fashionista” kuanzia audio hadi video.