Kampuni ya LG inajipanga kuachana na biashara ya simu na CEO wake Kwon Bong-seok amewajulisha wafanyakazi kuhusu mabadiliko mapya ambayo yataitoa LG katika biashara ya simu.
LG imepoteza zaidi ya dolla bilioni 4.5 na kuzidiwa soko na Samsung, Huawei, Apple, Xiaomi na Vivo; imeamua kuweka malengo katika biashara ya vifaa vingine kama vifaa vya majumbani.
Mabadiliko haya hayatachukua muda mfupi ili kuipa nafasi ya LG kuamua kuuza brands zake za simu na kupanga namna ambavyo watumiaji wake wataendelea kupata updates na support katika simu ambazo zipo tayari katika soko.