Mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka nchini Marekani Lebron james anayeichezea klabu ya lakers ni mmoja kati ya wachezaji wengi wanaopenda muziki.
Kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwenye muziki lebron james ameweka wazi mpango wake wa kuja na album ya rap, katika album hiyo hatochana ila ana mpango wa kuwakusanya wasanii mbalimbali wa rap ambao ni marafiki zake ili kukamilisha album hiyo.
Lebron james ameweka wazi mpango wake huo kupitia ukurasa wake wa Twitter na tayari mashabiki mbalimbali wameanza kuisubiri kwa hamu album hiyo huku watu wengi wakitarajia kumuona rapa Jay z ndani kwa sababu ni rafiki mzuri wa Lebron James.