LADY JAYDEE AICHIA ‘GOOD VIBES’

You are currently viewing LADY JAYDEE AICHIA ‘GOOD VIBES’
  • Post category:Burudani

Msanii tajika kutoka pande za Bongo Lady Jaydee ameachia single yake mpya inayokwenda kwa jina la Good Vibes Ijumaa hii.

Wimbo umetayarishwa na Tony Drizzy na kuandikwa na muimbaji huyo nguli akishirikiana na Tim Jackson aka Golden Child.

Kwenye Good Vibes, Jaydee ameonesha umahiri wake kwenye muziki wa Hiphop mwishoni mwa ngoma hiyo.

Wakati huo huo, hitmaker huyo ambaye jina lake halisi ni Judith Wambura Mbimbo, anajiandaa kuzindua album yake mpya, 20.

Uzinduzi wa album hiyo utafanyika Ijumaa ya February 12 mwaka huu, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa