Kundi la wasomi katika eneo la Nakwamekwi viungani mwa mji wa Lodwar wametoa msaada wa vyakula na bidhaa nyingine kwa familia maskini ambazo zimeathirika pakubwa na janga la corona katika kijiji cha Nataparkakono.
Mwenyekiti wa kundi la wasomi wa Nakwamekwi Francis Nakwar amesema wamechukua hatua hiyo kuzisaidia familia 250 zisojiweza katika eneo hilo baada ya shughuli zao ambazo walikuwa wanategemea kama kitega uchumi kusimamishwa kutoka na corona.
Aidha amesema wametumia hafla hiyo kutoa elimu kwa wakaazi kuhusu umuhimu wa kujikinga na virusi vya COVID-19 kwa kuosha mikono kila mara wakitumia maji tiririka na sabuni pamoja vitakasa.
Wakati uo huo wamewataka wananchi kuachana mila na desturi zitakazochangia kuenea kwa ugonjwa wa corona endapo utaingia kaunti hiyo huku wakitoa wito kwa serikali ya kaunti kusambaza maji katika eneo hilo ili kupiga jeki mapambano dhidi ya corona.
Hata hivyo wametoa wito kwa serikali kuu,ya kaunti na mashariki mengine ya kijamii kutoa msaada wa vyakula kwa wakaazi wa kaunti ya Turkana ambao wameathirika na janga la corona.