Rapa kutoka nchini tanzania Joh Makini amethibitisha kuwa Album mpya ya kundi la Weusi, inatarajiwa kutoka mwezi ujao tarehe 12.
Kundi la Weusi ambalo kwa sasa linafanya vizuri na kibao chao, cha ‘Penzi la Bando’ wakiwa na mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarab, Bi Khadija Kopa, tarehe 8 mwezi 3 wataachia orodha ya ngoma zinazopatikana ndani ya album hiyo ya “Air Weusi”
Sanjari na hilo, rapa Joh Makini kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kwamba album hiyo itapatikana kwenye digital platform zote kuanzia tarehe 12 mwezi 3, hivyo mashabiki kuanzia sasa wanaweza ku pre-order album ya “Air Weusi”.