KUNDI LA ABANGO NAAJOKHON LAWAVUTIA WENGI KAUNTI YA TURKANA KWA UBUNIFU WAO WA KUZALISHA  NYAMA YA MIKEBE KIASILI

KUNDI LA ABANGO NAAJOKHON LAWAVUTIA WENGI KAUNTI YA TURKANA KWA UBUNIFU WAO WA KUZALISHA NYAMA YA MIKEBE KIASILI

Kundi moja la akina mama linalojulikana kama Abango na Naajokon kwenye Kaunti ndogo ya Turkana Mashariki ambalo limejikita kwenye shughuli ya kuuza nyama ya mikebe iliyozalishwa kwa njia ya kiasili maarufu Arukot linaendelea kuwavutia wateja wengi kaunti ya turkana  na nje ya kaunti hiyo licha ya changamoto zinazoikabili.

Kulingana na Mkurungezi wa kitengo cha mauzo cha kikundi cha Abango Naajokon Bi Jessicah Iuren anasema kikundi hicho ambacho kilibuniwa Mwaka mmoja uliopita kimewaleta pamoja wanawake kumi na moja kutoka Kaunti ya Turkana ambapo kwa sasa wanajishughulisha na biashara ya utengezaji na uuzaji wa nyama ya mikebe kwa njia ya asili maarufu Arukot

Aidha Bi Iuren amesema licha ya changamoto zinazowakabili kwenye suala la kutafuta soko, wameanza kuwavutia watu mbali mbali Kaunti ya Turkana wakiwemo wafanyikazi wa Mashirika na Shule zilizoko Kaunti ndogo za Turkana Mashariki na Kusini.

Ni mpango ambao ni wa kipekee Kaunti ya Turkana ambao kwa sasa umewavutia viongozi wakuu wa kaunti hiyo akiwemo Gavana Josphat Koli Nanok ambaye amefurahishwa na ubunifu wa akina mama hao akisema Serikali ya Kaunti itaendelea kuunga mkono juhudi za wafanyibiashara wadogo ili waweze kuendeleza shughuli zao bila kizingiti.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts