Rapa kutoka Marekani Kodak Black ni mwingi wa kushukuru, amehamua kuchora tattoo kiganjani yenye jina la mwanasheria wake Bradford Cohen kama shukrani kwa kufanikiwa kumtoa gerezani.
Kodak Black alikuwa miongoni mwa wafungwa waliopatiwa msamaha na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump, wiki iliyopita. Rapa huyo alikuwa akitumikia kifungo cha miezi 46 gerezani kwa makosa ya kugushi nyaraka za Serikali kujipatia silaha.