Kiwanda cha nyama cha Nasukuta iliyoko eneo la Chepareria eneo bunge la Pokot Kusini kitaleta manufaa mengi kwa wakaazi wa kaskazini mwa Bonde la ufa
Waziri wa kilimo kaunti ya Pokot Magharibi Geofrey Lipale anasema kwa muda sasa wengi wa wananchi wamekuwa wakisafiri mwendo mrefu kuuza mifugo wao na hali hiyo imerahisishwa
Aidha amesema kupitia kiwanda hicho wananchi watanufaika na bei nzuri kuzidisha juhudi za kupatikana kwa soko nzuri kwa mifugo,kubuni nafasi za ajira kwa vijana na kuinua uchumi wa kaunti
Hata hivyo ameongeza kuwa kupitia biashara mipakani itachochea ushirikiano mwema kudumisha amani ambayo imekuwapo kwa muda sasa