KISA CHA MWANAHABARI WA GAZETI LA THE STAR KUSHAMBULIWA TURKANA CHAIBUA HISIA MSETO MIONGONI MWA VIONGOZI MBALI MBALI

KISA CHA MWANAHABARI WA GAZETI LA THE STAR KUSHAMBULIWA TURKANA CHAIBUA HISIA MSETO MIONGONI MWA VIONGOZI MBALI MBALI

Kisa cha Mwananabari wa Gazeti la The Star Hesbon Etyang kushambuliwa na wafanyikazi wa hoteli ya Stegra mjini Lodwar baada ya kupiga picha tukio la mtoto wa miaka 10 kutumbukia kwenye kidimbwi cha kuogelea hoteli humo linaendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa viongozi mbali mbali kaunti ya Turkana.
Akizungumza na Northrift radio mjini Lodwar Mwenyekiti wa Baraza la Muungano wa Madhehebu ya Kidini Kaunti ya Turkana Yusuf Aremons amesikitishwa na kitendo cha kuumizwa kwa wanahabari huyo ambaye alikuwa akifuatilia kisa cha mtoto aliyekuwa amezama kwenye kidimbwi cha maji katika hoteli ya Stegra.
Aidha Aremons amezitaka vyombo vya usalama kuanzisha uchunguzi na kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika waliotekeleza kitendo hicho  huku akitoa wito kwa hoteli zote kwenye Kaunti ya Turkana zilizo na vidimbwi vya kuogelea kuwa na wapiga mbizi waliohitimu kuzuia visa vya watu kufa maji.
Kwa sasa mwanahabari huyo ameruhusiwa kwenda nyumbani baada kupokea matibabu huku mtoto aliyenusurika kufa maji kwenye kidimbwi cha kuogelea katika hoteli ya Stegra mjini Lodwar akiendelea kupokea matibabu kwenye Hospitali yaRufaa ya Lodwar.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts