Serikali ya kaunti ya turkana imezindua rasmi usambazaji wa chanjo ya virusi vya corona.
Akizungumza alipoongoza hafla ya uzinduzi wa chanjo hiyo, naibu gavana kaunti ya turkana Peter Lotethiro amesema Kipau mbele katika utoaji wa chanjo hiyo itapewa wahudumu wa afya, maafisa wa usalama , walimu watu walio na umri mkubwa na wale walio na kinga dhaifu kabla ya kusambazwa kwa wakaazi wote wa kaunti hiyo.
Kwa upande wake waziri wa afya Jane Ajele amesema kupatikana kwa chanjo ya Corona sio ishara ya kumalizika kwa maradhi ya COVID-19 hivyo kuwasihi wakaazi wa turkana kuzidi kuwa makini katika kukabiliana na maradhi hayo.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Afisa mkuu katika wizara ya Afya kaunti hiyo Augustine Lokwang ambaye amedokeza kuwa chanjo hiyo ndio silaha itakayosaidia kupambana na virusi vya corona.
Haya yanajiri baada ya taifa kupokea dozi milioni 1.02 za chanjo ya Oxford-AstraZeneca Jumatano wiki iliyopita.