Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi John Lonyangapuo ameelezea utayari wa kaunti yake kukabiliana na virusi vya Corona endapo itatangazwa.
Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya kipekee Lonyangapuo amesema tayari vitanda 10 vya wagonjwa mahututi vimetengwa katika hospitali ya Rufaa ya Kapenguria huku pia vituo tofauti vikitengwa katika maeneo mbalimbali kaunti hiyo.
Aidha amekiri kuwepo na changamoto ya kifedha akisema wengi wakaazi wa kaunti ya Pokot Magharibi kwa sasa wanakabiliwa na makali ya njaa baada ya kutii agizo la serikali la kusalia majumbani kutokana na tishio la Corona.