Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi imetakiwa kuweka mikakati zaidi ili kuzidisha uzalishaji wa chakula katika wadi mbali mbali kaunti hiyo.
Akizungumza kwenye kikao kilichowaleta pamoja washikadau mbali mbali katika eneo la KBC Lutheran, mdhamini wa kikao hicho kutoka shirika lisilo la kiserikali k. a. s {Konrad Adenua Stiftung) na ambaye ni mkurungezi mkuu wa shirika hilo nchini Kenya, Dr. Annette Cchwander, anasema kuwa swala la uzalishaji wa chakula linafaa litiliwe maanani.
Kadhalika msimamizi wa miradi nchini kwenye shirika hilo bwana Duncan Odele, amesema kwamba kikao hicho kitatoa mafunzo kwa washikadau ili waeneze ujumbe huwo kwenda kwa jamii
Kulingana na Duncan, watazidi kushirikiana na serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi ili kutafta suluhu mwafaka ya kupunguza utapia mlo kwenye wadi kadhaa kaunti hiyo.
Ikumbukwe kilele cha kikao hicho kitakuwa hapo kesho ambapo Gavana John Lonyangapuo anatarajiwa kuhudhuria.