Rapa kutoka nchini Marekani Kanye West anaamini sababu za mkewe Kim Kardashian kudai talaka ni kutokana na yeye kuutaka Urais wa Marekani mwaka 2020.
Juzi kati Kim Kardashian aliwasilisha mahakamani ombi la talaka kutaka kuachana na Kanye West.
Baada ya tamko hilo, Kanye West alianza kuwatumia watu ujumbe mfupi na wengine kuwapigia simu akizungumzia ishu hiyo.
Mtandao wa PEOPLE umeripoti kwamba malalamiko makubwa ya kanye West yamekuwa kwenye majuto, moja wapo likiwa la kuwania Urais wa Marekani kwa sababu Kim kardashian hakumtaka afanye jambo hilo.