Mtaala mpya wa elimu CBC huenda ikakosa kuafikia malengo yake humu nchini kutokana na changamoto za kifedha.
Kulingana na mmoja wa wasomi katika kaunti ya Pokot Magharibi John Ng’imor ili kufanikisha mtaala huo fedha nyingi zitahitajika kuboresha miundo msingi sawa na kuchapisha vitabu vya gredi mbalimbali.
Aidha anasema walimu wataofundisha mtaala huwo ni wachache mno huku pia akiibua maswali kuhusu hatma ya walimu wengi ambao walipata mafunzo kupitia mtaala wa 8-4-4.