Wanachama wa Barcelona walimchagua Joan Laporta kama rais wa klabu siku ya Jumapili.
Laporta, ambaye alikuwa rais wa Barça kati ya 2003 na 2010, alishinda kwa kupata asilimia 57.6% ya kura, wakati Victor Font akiwa wa pili kwa 31.8% na Toni Freixa wa tatu kwa 9.1%.
Laporta, ambaye ahadi yake kuu ni kuhakikisha Lionel Messi anaendelea kuwepo klabuni hapo anamrithi Josep Maria Bartomeu, ambaye alijiuzulu kama rais mnamo Oktoba 2020.
Messi alikuwa miongoni mwa wachezaji kadhaa wa Barça waliopiga kura katika uchaguzi siku moja baada ya kushinda 2-0 huko Osasuna na kushika nafasi ya pili La Liga.