Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Jimmy Gait amefunguka sababu za kutoingia kwenye ndoa.
Akiwa kwenye moja ya interview Jimmy Gait amesema licha ya kutamani kuwa na familia, bado ana uvumilivu kwenye mchakato wa kumtafuta mwanamke wa ndoto yake kwani anamini ataingia kwenye ndoa muda sahihi ukifika.
Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kwamba kuna kipindi alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka mitano akiwa na matumaini yangempelekea kuingia kwenye ndoa lakini mwisho wa siku mahusiano hayo yalivunjika.
Kulingana na Jimmy Gait, tatizo kubwa ambalo amekutana nalo ni kumpata mtu sahihi wa kuingia nae kwenye ndoa ikizingatiwa kuwa baadhi ya watu huingia kwenye mahusiano kwa faida zao za kibinafsi.
Hata hivyo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Makuu” amesema anaamini atampata mwanamke wa ndoto yake katika siku za hivi karibu licha ya kupata shinikizo kutoka kwa watu wake wa karibu.