JIMBO KATOLIKI LA LODWAR LINAKADIRIA HASARA BAADA YA MAFURIKO KUSOMBA MALI YA MAMILIONI YA PESA

Ukumbi wa mikutano wa St Teresa unaomilikiwa na Jimbo Katoliki la Lodwar unakadiria hasara baada ya mafuriko kusomba mali ya mamilioni pesa.

Kulingana na Msimamizi wa ukumbi huo Mtawa Salome Cherono amesema juhudi za uokozi zilingonga mwamba baada ya maji kuwa mengi  na kuharibu majumba mengi ya mikutano iliyokuwa na mali ya mamilioni ya pesa.

Kwa upande wake Mshirikishi wa Idara ya Mawasiliano katika Jimbo Katoliki la Lodwar Kasisi Ignatius Mwinamo ametoa wito kwa hisani na waumini wa majimbo mengine ya kanisa katoliki nchini kuingilia kati na kusaidia kuikarabati ukumbi huo kwani ni kitega uchumi kwa jimbo hilo.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts