Siku chache zilizopita WhatsApp ilitangaza kubadilisha sera yake ya faragha na kuunganisha data zinazokusanywa na WhatsApp pamoja na Facebook. Kutokana na hilo India imeitaka Facebook kuacha kufanya mabadiliko ya kuunganisha data za watumiaji wa WhatsApp na Facebook na itoe ufafanuzi na ushahidi kuhusu uhifadhi na matumizi ya data za watumiaji wanaoishi India.
Ikumbukwe India ni nchi inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi wa WhatsApp duniani kwa zaidi ya watumiaji Million 480 (kwa ripoti za mwaka jana) wanatumia app ya WhatsApp kila siku.
Hii itakuwa ni habari mbaya kwa WhatsApp, hasa ukizingatia India ipo makini sana na apps na kama iliweza kuifungia TikTok, WeChat na apps nyingi kubwa kutokana na uwepo wa watumiaji wengi wanaotumia simu.
Hata hivyo India imetaka maelezo ni kwanini Umoja wa Ulaya watumiaji wake hawatopata mabadiliko haya lakini sera hii mpya itakuwepo India.