IDADI YA WATOTO WALIOPOKEA CHANJO YA POLIO TURKANA YAONGEZEKA

IDADI YA WATOTO WALIOPOKEA CHANJO YA POLIO TURKANA YAONGEZEKA

Zaidi ya asilimia  105 ya watoto chini ya umri wa miezi 9 na miaka kumi na nne wamepokea chanjo ya Polio katika kaunti ya Turkana. Hii ikiwa ni asilimia tano zaidi ikilinganishwa na kiwango kilichotarajiwa cha asilimia mia moja kwenye zoezi la siku tano la utoaji chanjo lilokamilika mwezi disemba mwaka jana.

Akitoa ripoti ya chanjo hiyo Waziri wa Afya Jane Ajele amesema kuwa watoto elfu 198,000 wamepokea chanjo hiyo ikilinganishwa na watoto 131,709 waliolengwa.

Eneo la Turkana Magharibi ndilo liliripoti idadi kubwa ya watoto waliochanjwa, ikiwa na watoto elfu 57,839 ikifwatiwa na Turkana ya Kati,ambayo ilirekodi watoto elfu 40,000. Loima, watoto elfu 26,980 walichanjwa, Turkana Kusini, watoto elfu 31,000 na Turkana Mashariki watoto elfu 18, 887.

Aidha katika eneo la Turkana Kaskazini, watoto elfu 16,000 walichanjwa, huku Kibish ikiripoti watoto elfu 10,153 waliochanjwa

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts