Staa wa muziki nchini Tanzania, msanii Harmonize amewahimiza wasanii wa Bongo fleva kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao.
Harmonize ambaye amepata mafanikio makubwa kupitia nyimbo zake 2, ambazo ni ‘Bedroom’ na ‘Falling in Love’ alizoimba kwa lugha hiyo, amesema lengo kuu ni kuutangaza muziki wa bongofleva kimataifa.
Ikumbukwe Harmonize kwa sasa yupo mbioni kuachia album yake mpya ambayo amesema itakuwa na nyimbo ambazo ameziimba kwa lugha ya kiingereza.