Baada ya kuvuja kwa picha za zilizotafsiriwa kutokuwa na maadili za msanii wa bongofleva Rayvanny na Binti wa mwigizaji Bongo movie Kajala’, sasa mwigizaji huyo amemtupia lawama msanii huyo na mwanamitindo wa nchini tanzania Hamisa Mobetto.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwigizaji Kajala ameeleza kuwa Hamisa mobeto alipanga njama na kufanikisha mazingira ya Rayvanny kutoka kimapenzi na bintiye huku akiomba msaada wa mamlaka husika kuchukua hatua juu ya suala zima.
Hata hivyo Hamisa Mobeto amejibu tuhuma hizo za moja kwa moja kutoka kwa Kajala, akieleza kuwa anaweza kulaumiwa kwa kukubali ombi la kumtoa binti wa kajala kwa ajili ya kupata mlo wa mchana na sio vinginevyo.
Hata hivyo, Hamisa pia ameongeza kuwa hatakubali kuchafuliwa jina juu ya picha zisizo na maadili kati ya Rayvanny na binti wa kajala huku akisema kuwa atachukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaomuharibia sifa.