Rapa kutoka nchini Uganda Gravitty Omutujju amefunguka sababu za kutomuunga mkono msanii Jose Chameleone kwenye kinyanganyiro cha umeya wa Jiji la Kampala katika uchaguzi uliokamilika majuzi nchini humo.
Akiwa kwenye moja ya Interview Omuttujju amesema mwanamuziki huyo hakuwahi kuomba uungwaji mkono kutoka kwake, hivyo wakati mpinzani wake Erias Lukwago alipokuja kumuomba usaidizi wake hakuwa na budi ya kupigia debe kwenye kinyanganyiro cha umeya.
Hata hivyo amekana taarifa zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana ugomvi na Jose Chameleone huku akisema kuwa hana utofauti wowote na msanii huyo licha ya kutomuunga mkono kwenye uchaguzi wa umeya wa Jiji la Kampala uliokamilika.