GLORIA MULIRO ATHIBITISHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MPYA.

You are currently viewing GLORIA MULIRO ATHIBITISHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MPYA.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Gloria Muliro amethibitisha kuingia kwenye mahusiano mapya na mwanaume wa ndoto yake ikiwa ni miaka sita baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Pastor Eric Omba.

Akipiga stori na gazeti moja nchini Gloria Muliro ambaye anafanya vizuri wimbo wake mpya uitwao “Anatenda” amethibitisha kufunga ndoa nyingine na kasisi aitwaye “Evans Sabwami” na tayari wamefanya harusi ya kitamaduni.

Aidha ameenda mbali zaidi na kusema  kwamba  sasa hivi wana mpango wa kuandaa harusi ya kanisani kukamilisha mchakato wa kuhalalisha ndoa yao.

Ikumbukwe Gloria muliro alifunga ndoa na Pastor Eric Omba mwaka wa 2009 lakini walikuja wakaachana mwaka wa 2015 baada ya ndoa yao kuingiwa na ukungu.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa