Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi John Krop Lonyang’apuo amekariri msimao wake wa kuinua uchumi wa kaunti hiyo kulingana na ajenda ya serikali yake.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zaidi ya vijana 100 wa chama cha ushirika cha kifedha maarufu WEPESA katika eneo la Chepareria, Profesa Lonyang”apuo ameelezea haja ya wakaazi kaunti hiyo kujiunga na vyama vya ushirika kama njia moja ya kujikwamua kutoka lindi la umaskini sawa na kuinua uchumi wa kaunti.
Aidha Lonyang’apuo ametoa wito kwa wakulima na wafanyibiashara kutumia fursa ya chama hicho cha wepesa kuchukua mikopo ya kuendeleza na kupanua biashara zao huku akisifia utendakazi wa serikali yake ya kusaidia wenyeji.