Kampuni ya Facebook imesema itarejesha maudhui ya taarifa za Habari kwa Watumiaji Nchini Australia baada ya kuyafungia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Facebook ilichukua hatua hiyo kufuatia mvutano kuhusu upendekezaji wa Sheria ambayo italazimu Mtandao huo pamoja na Google kuwalipa wachapishaji wa habari kwa taarifa zao.
Serikali ya Australia na Facebook zimetangaza kufikia makubaliano baada ya mazungumzo kadhaa kati ya pande hizo mbili.